18 Simba wanakiwasha tena, Chikwende aondolewa

LICHA ya baadhi ya nyota wake kurejea jijini Dar es Salaam, lakini unaambiwa kikosi cha wachezaji 18 waliosalia kambini mjini Rabat, Morocco wanaendelea kukiwasha kama kawaida na kati ya leo na kesho watarudi tena uwanjani kucheza mchezo wao wa pili wa kirafiki wa kimataifa.

Awali, Simba iliyo chini ya Kocha Didier Gomes, ilikiwasha kutesti mitambo dhidi ya FAR Rabat na kutoka sare ya 2-2, huku Wekundu wa Msimbazi wakilazimika kuchomoa kipindi cha pili kupitia kwa Hassan Dilunga na Pape Sakho. We are waiting for the next game to try online betting .

Mwanaspoti limeelezwa wachezaji waliokuwa kambini awali zaidi ya 30, ila sasa wamebaki 18, wanaoendelea na mazoezi baada wengine kuwa katika timu zao za taifa. Kwenye maandalizi ya msimu ujao amebaki kipa mmoja, Ally Salim ambaye ratiba yake inaonyesha huanza mazoezi na kocha wa makipa Milton Nienov kisha baadae hucheza na wachezaji wengine ambayo huwa chini ya Gomes. Kipa mwingine Beno Kakolanya aliondoka alipofiwa na mama yake, Aishi Manula yupo Taifa Stars na Jeremiah Kisubi aliyeshindwa kusafiri na kikosi hicho.

Inaelezwa Salim amekuwa katika kiwango bora na ndiye atakayesimama langoni kama alivyofanya dhidi ya Far Rabat inayonolewa na kocha wa zamani wa Simba, Sven Vandenbroeck, huku ikielezwa huenda suala lake la kwenda kwa mkopo likawa gumu kutokana na kumvutia zaidi Gomes.

Salim kama atacheza vizuri mechi hizo mbili za kirafiki kama kiwango alichoonyesha mechi ya kwanza analezwa atapewa nafasi ya kucheza michezo mingine ya mashindano.

Kipa huyo na wenzake waliobaki ndio watacheza mechi mbili zilizobaki za maandalizi na kundi la mwisho kutoka Morocco litarejea Septemba 4.

Wachezaji 18 wanaoliamsha kambini ni Salim, Peter Banda, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Pape Ousmane Sakho, Chriss Mugalu, Pascal Wawa, Jimsony Mwanuke, Sadio Kanoute, Duncan Nyoni, Hennock Inonga Baka ‘Varane’, Yusuph Mhilu, Abdulsamad Kassim, Gadiel Michael, Bernard Morrison, Larry Bwalya, Joash Onyango na Ibrahim Ajibu.

Wachezaji hao wanaendelea na ratiba ya mazoezi awamu mbili – asubuhi huingia gym kufanya mazoezi mengi ya nguvu na husimamiwa na kocha wa viungo, Adel Zrane kisha awamu ya pili huwa jioni ambayo hufanya ya kiufundi zaidi uwanjani na shoo nzima huwa chini ya Gomes na msaidizi wake Selemani Matola.

CHIKWENDE AONDOLEWA

Katika hatua nyingine winga wa Simba, Perfect Chikwende aliyekuwepo kambini, wiki iliyopita alipatiwa taarifa ya kutolewa kwa mkopo.

Kiongozi mmoja aliyepo Rabat aliliambia Mwanaspoti baada ya suala la Chikwende kurudishwa kwa mkopo FC Platinum ya Zimbabwe kuwa gumu waliamua vingine.

Uamuzi ambao viongozi waliufanya ni kuangalia timu ambayo inaweza kumpatia maslahi mazuri ili wapunguze gharama za kumlipa.

“Timepata moja ya timu iliyopo Afrika Kusini na tayari tumekubaliana nao kumchukua Chikwende ili kwenda kuwatumikia, kwa maana hiyo mambo yakiwa tayari tutaeleza ni timu gani,” alisema.

“Chikwende msimu ujao atakuwa huko Afrika Kusini kwenye hiyo timu, tunaogopa kuiweka wazi kutokana suala lake kuwa bado halijamalizika. Kwa hiyo tunaweza kwenda tofauti na dili hilo likashindwa kufanikiwa. Tumeamua kumuacha kwa mkopo.”

About the author

Antonie Meeker

Antonie Meeker is a chief content editor for Mechanicfaq. He is an avid adventure hunter and loves to ride his ATV anywhere he can. He lives with his girlfriend and their cat named Moe.

Leave a Comment